Mapigano ya M23 yasababisha majeruhi na wakimbizi DRC

CONGO : MAKUMI ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi kulazimika kuhama makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mapigano ya jeshi la Congo na wapiganaji wa M23.

Hayo yameelezwa na vyanzo vya ndani pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali. SOMA: Wakazi laki moja wakimbia makazi Congo

Kundi la M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, ambalo sasa linachukuliwa kama kundi la kigaidi na serikali mjini Kinshasa, limechukua udhibiti wa maeneo mengi mashariki mwa DRC, eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali na lililokumbwa na migogoro kwa miaka 30.

Katika wiki za hivi karibuni, kundi hilo la waasi wa M23 limepata nguvu zaidi na mapema mwezi huu lilidhibiti mji mkuu wa eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Jeshi la Congo limeapa kuchukua tena udhibiti wa maeneo yote na limekuwa likifanya mashambulizi ya kukabiliana na kundi hilo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button