Wakazi laki moja wakimbia makazi Congo

CONGO : UMOJA wa Mataifa umesema mapigano yanayoendelea katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamepelekea zaidi ya watu 100,000 kugeuka wakimbizi ndani ya kipindi cha wiki moja.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa umesema kati ya tarehe 1 hadi 3 Januari, mapigano kati ya jeshi na waasi wa M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini, yamesababisha watu kuhama 102,000.
Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda inadai kuwa eneo lililotwaliwa na waasi wa M23 hivi karibuni lilikuwa kwenye mikono ya wanamgambo wa Kihutu, FDLR, wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.
SOMA: DR CONGO : ADF yaua watu 12 Congo
Kwenye taarifa yake, Waziri wa Mambo ya nje nchini Rwanda, Olivier Nduhungirehe, alilaani kuvamiwa huko kwa mamlaka ya ardhi ya Kongo inayomililiwa na jamii za Wakongo, wakiwemo Watutsi wa Kikongo.


