CONGO : MAPIGANO yamezuka tena kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huko Mashariki mwa nchi hiyo.
Mapigano haya yamevunja makubaliano ya usitishwaji wa mapigano ambayo yamedumu kwa wiki kadhaa.
Jumapili ya wiki hii kikundi cha waasi wa M23 walipambana na wanamgambo wazawa na kuwajeruhi raia 14 wakiwemo vijana wawili.
Usitishaji wa mapigano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 unaungwa mkono na Rwanda kufuatia mazungumzo ya upatanishi yaliyofanyika nchini Angola.
Hapo awali mazungumzo ya amani kati ya Kinshasa na Kigali yalikwama lakini mazungumzo mengine yamepangwa kufanyika mjini Luanda mwishoni mwa wiki ijayo.
Tangu M23 ilipoanzisha mashambulizi mapya iliamua kuteka maeneo makubwa yaliyopo mashariki mwa Kongo ambayo yanadaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini .