Marcus Rashford mambo sio shwari Old Trafford
TETESI za usajili zinasema wawakilishi wa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, wamekutana na viongozi wa Barcelona huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akitafuta njia ya kuondoka Old Trafford. (Sky Sports)
Arsenal imefanya ulizo la awali kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Slovenia mwenye umri wa miaka 21, Benjamin Šeško, kutoka klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani. (Talksport)
AC Milan imekubaliana dili la kumsajili beki wa Manchester City, Kyle Walker mwenye umri wa miaka 34 ambalo litakuwa mkopo wa awali lakini likijumuisha chaguo la kumnunua kwa pauni milioni 4.2. (Sky Sports Italy)
Mazungumzo ya Arsenal na Juventus kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24 yamevunjika. (Football Transfers)
Napoli pia ipo kwenye mazungumzo kuhusu kumsajili winga wa Borussia Dortmund ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, Karim Adeyemi. (Fabrizio Romano)
Wachezaji watatu wa Chelsea wanaweza kuondoka mwezi huu, huku beki wa Ureno, Renato Veiga, mwenye umri wa miaka 21, akishinikiza kujiunga na Juventus, kiungo wa Italia Cesare Casadei, mwenye umri wa miaka 22, akiwa kwenye rada ya Lazio baada ya ofa ya pauni milioni 11.5 na beki Ben Chilwell, mwenye umri wa miaka 28, akiwaniwa na klabu ya Everton. (Mail)



