MAREKANI : BARAZA Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kutaka kusitishwa mara moja na bila masharti mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Wanachama 158 walipiga kura kuunga mkono azimio hilo, tisa walipinga na 13 walijizuia kupiga kura.
Azimio la kusitisha mapigano bado limekataliwa na serikali ya Marekani na Israel licha ya wajumbe wengi kuunga mkono.
Baraza hilo pia limeidhinisha azimio jingine linalounga mkono Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.
Hatahivyo, Baraza hilo lilisikitishwa na kitendo cha Israel kupitisha sheria mpya ambayo inapiga marufuku shughuli za shirika hilo nchini Israel kuanzia mwishoni mwa mwezi Januari.
Wakati huohuo, shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limeripoti kuwa mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu wapatao 33, wakiwemo walinzi 12 wanaolinda malori ya misaada kwenye maeneo ya kusini mwa Mamlaka ya Palestina.
SOMA: Israel yashtumiwa kuhusika mauaji halaiki Gaza