Marekani kuondoa wanajeshi Niger

NIGER : SERIKALI ya Marekani imetangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger kwa awamu.

Uamuzi huu umekuja baada ya Serikali ya Niger  kutoa agizo kwa Serikali ya Marekani kuondoa wanajeshi na watumishi wengine  wapatao 1000 nchini humo

Hatahivyo Serikali  ya Marekani imesema  itanedelea kutoa mafunzo kwa vikosi vya Niger ili kuwasaidia kukabiliana na ugaidi wa makundi ya dola la Kiislamu na al Qaeda katika eneo hilo.

Kabla ya mapinduzi, Niger ilikuwa mshirika mkubwa wa Marekani katika vita dhidi ya uasi katika ukanda wa Sahel, na kusababisha vifo vya maelfu na wengine mamilioni kukimbia makazi yao.

Washington inaangazia mpango mbadala katika eneo la Afrika Magharibi lakini mchakato huu unakwenda taratibu.

SOMA :Wanajeshi wanaotaka kujitenga waua watu 11 Nigeria

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button