MAREKANI : Moto mpya wazuka Calirnia

MAREKANI : MAELFU  ya wakazi kusini mwa mji wa California wametakiwa kuondoka baada ya kuzuka moto mpya wa nyika, kaskazini mwa Los Angeles.

Moto huo, unaojulikana kama Hughes Fire, umesambaa kwa haraka takriban kilomita za mraba 41, na unawaka karibu na eneo maarufu la burudani la Ziwa Castaic, ambalo liko takriban kilomita 64 kutoka eneo lingine lililokumbwa na moto mkubwa uliozuka Januari 7 na bado haujazimwa kikamilifu.

Mkuu wa polisi katika kaunti ya Los Angeles, Robert Luna, alisema zaidi ya watu 31,000 wameagizwa kuondoka hadi sasa.

Alisema,“Idadi ya watu 31,000 tayari wanatakiwa kuhama, na wengine 23,000 wataathirika watafuata ,” alisema Luna. SOMA: Moto Los Angeles waua watu 24

Hadi sasa, bado haijajulikana ikiwa kuna mali zilizoharibiwa na moto huo mpya, huku watu wakiendelea kushughulikia athari za ghasia za moto unaoendelea.

Moto huu unaongezeka katika hali ya wasiwasi, huku mamlaka za usalama zikiendelea kufanya juhudi za kukabiliana nazo.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button