Moto Los Angeles waua watu 24

MAREKANI: IDADI ya watu waliokufa kutokana na moto wa nyika ulioanza tangu Januari 7 huko Los Angeles, Marekani, imefikia 24.

Mkuu wa Idara ya Zimamoto, Anthony Marrone, ametahadharisha umma kuwa moto mpya unaweza kuzuka kutokana na upepo mkali. SOMA: Kimbunga Milton chabisha hodi Florida

“Maelfu kwa maelfu ya vitu vinavyowaka, tena mapande makubwa makubwa yanapeperushwa na upepo, na hii inaweza kusambaza moto zaidi,” alisema Marrone.

Advertisement

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Marekani (White House), watu 24,000 wamejiandikisha ili kupatiwa msaada kufuatia maafa hayo.

Moto huo umeteketeza makazi ya watu na kuharibu kabisa mji wa Los Angeles, uliopo katika jimbo la California, na kuwaacha maelfu ya watu bila makazi.