MAREKANI : KIMBUNGA Milton kimetuwa jimboni Florida na kusahabisha uharibifu mkubwa na kuacha takriban nyumba na maakazi milioni 3 bila ya huduma ya umeme .
Kampuni za nishati ya umeme zimeendelea kutoa huduma kwa takriban watu milioni 11.5 huku idadi inayoongezeka ya watu wakiendelea kukosa umeme kutokana na kiwango cha juu cha upepo, dhoruba kali na mvua kubwa ikiendelea kunyesha kutokana na athari za kimbunga Milton.
Haya yanajiri huku Rais Joe Biden akimshambulia Donald Trump kwa madai ya kueneza taarifa za uongo juu ya jinsi serikali yake ilivyolishughulikia suala la Kimbunga.
SOMA : Mamia ya watu hawajulikani walipo
Kimbunga Milton kimetuwa Florida na kinatajwa kuwa kikali na cha hatari zaidi, kikipiga kwa kiwango cha juu zaidi ukilinganisha na Kimbunga Helene.