Marekani imefuta deni dola bilioni 1 Somalia

MAREKANI : SERIKALI ya Marekani imeamua kufuta deni la zaidi ya dola bilioni 1 ambazo zinadaiwa kwa serikali ya Somalia.

Makubaliano ya kufuta deni hilo yalisainiwa kati ya Waziri wa Fedha wa Somalia Bihi Egeh na Balozi wa Marekani nchini Somalia Richard Riley.

Wakati wa hafla hiyo ya utiaji wa saini, Riley amesema msamaha huo ni sehemu ya zaidi ya deni la jumla la dola bilioni 4.5 zinazodaiwa.

Advertisement

Aidha ameongezea kuwa msamaha huo ulipitishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia tangu mwezi Desemba.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha nchini Somalia Bihi Egeh amesema  msamaha huo utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini Somalia .

Hatahivyo, Ubalozi wa Marekani umesema msamaha huo wa deni ni mbali na dola bilioni 1.2 za misaada ya kimaendeleo, kiuchumi, kiusalama na misaada mingine ya kibinadamu ambayo Marekani imetoa kwa Somalia.

SOMA : Somalia yafutia deni la Dola milioni 4.5