Marekani yampa 5 Rais Samia kukuza Demokrasia

MAREKANI imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha na kukuza Demokrasia nchini

Makamu wa Rais Kamala Harris akizungumza leo Machi 30, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam amempongeza Rais Samia kuondoa zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

Pongezi hizo za Kamala, zimekuja zikiwa zimepita siku 87 tangu Rais Samia kuondoa zuio hilo Januari 3, 2023, lililodumu kwa miaka sita, tangu mwaka 2015.

Akiondoa zuio hilo Rais Samia alisema ‘Hii ni haki kwa sheria zetu, ni haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara’, uwepo wangu leo mbele yenu ni kuja kutangaza, lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoka.”

Pia, Kamala alimpongeza Rais Samia kuboresha uhuru wa vyombo vya habari.

“Kuhusu suala la usalama nashukuru kwa mchango wa Tanzania katika kuleta amani na usalama katika ukanda huu. Mimi na wewe tutajadili athari za vita vya Urusi nchini Ukraine kwenye usambazaji wa chakula na jinsi tunavyoweza kuisaidia vyema Tanzania katika juhudi zake za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya tabia nchini na ustahimilivu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x