Martha Karua kumtetea Besigye

KAMPALA : WAZIRI wa zamani wa sheria nchini Kenya Martha Karua, yuko nchini Uganda kuongoza timu ya mawakili wanaomtetea mwanaharakati wa kisiasa wa upinzani Dkt. Kizza Besigye na mshirika wake wa kisiasa, Hajj Obeid Lutale, katika mahakama ya kijeshi mjini Kampala.

Besigye na Lutale walitekwa nyara na idara za usalama za Uganda mnamo Novemba 16 jijini Nairobi, ambapo walikuwa wamesafiri kuhudhuria uzinduzi wa kitabu na Martha Karua.

Siku nne baadaye, wawili hao walifikishwa katika mahakama kuu ya kijeshi mjini Kampala, ambapo walishtakiwa kwa makosa manne yanayohusiana na usalama, kumiliki bastola mbili na risasi nane kinyume cha sheria. SOMA: KENYA: Odinga apewa saa tatu kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani

Wiki iliyopita siku ya Jumatatu, wakili kiongozi wa Besigye na Meya wa Kampala, Erias Lukwago, alitangaza kwamba Karua atachukua nafasi yake kama wakili mkuu.

Habari Zifananazo

Back to top button