Mashambulizi Israel yaua watu 492

LEBANON : ISRAEL imezidisha vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon Septemba  23, huku vita hiyo ikiua zaidi ya watu 490 na kujeruhi wengine zaidi ya 1,650 katika mashambulizi makubwa ya anga ambayo yamezua wasiwasi wa kutokea vita vikali.

Jeshi la Israel lilishambulia zaidi ya ngome 1,300 ambapo  shirika la habari la serikali ya Lebanon likiripoti mapigano makali katika majimbo mengi eneo la kusini mwa nchi.

Katika ripoti iliyotoka kwa Maafisa wa wizara ya afya ya nchini  Lebanon inaonyesha miongoni mwa waliouawa katika  vita hiyo  ni watoto 35 na wanawake 58.

Advertisement

Pia Jeshi la Israel limeonya wakazi wa bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon kukaa mbali na ghala za silala za Hezbollah.

Msemaji wa jeshi la Israel Amirali Daniel Hagari aliwambia waandishi wa habari kuwa wanaendelea na maandalizi ya Hezbollah uwanjani ili kuzuia mapema mashambulizi yao kwenye eneo la Israel.

SOMA :Israel yashambulia Lebanon

Katika ujumbe uliorekodiwa kwa raia wa Lebanon, waziri mkuu wa Israel Banjamin Netanyahu amewataka kuzingatia wito wa Israel wa kuondoka, akisema lazima “wachukulie onyo hilo kuwa sio mzaha.

/* */