MIAMBA ya soka nchini, Simba inashuja dimbani ugenini kuikabili Mashujaa katika mchezo pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
SOMA: Simba presha inapanda, inashuka
Kwa mara ya mwisho timu hizo kukutana katika mchezo wa Ligi Kuu Machi 15, 2024, Simba iliibuka mshindi kwa mabao 2-0.
Simba ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 baada ya michezo nane wakati Mashujaa ni ya saba ikiwa na pointi 13 baada ya mechi nane pia.