Matokeo kura za maoni UWT Manyara

MANYARA: Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, amemtangaza Regina Ndege kuongoza kura za maoni za nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara baada ya kujizolea kura 891 kati ya zaidi ya kura 1000 zilizopigwa.

‎Pia alimtangaza Yustina Rahhi kushika nafasi ya pili Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya akupata jumla ya kura 703.

‎Katika uchaguzi huo uliowakutanisha wagombea nane kutoka wilaya za mkoa wa Manyara,  mchuano huo wa kisiasa uliofanyika kwenye ukumbi mpya wa CCM Mkoa wa Manyara.

‎Chama Cha Mapinduzi kimeeleza kuridhishwa na utaratibu wa uchaguzi huo na kupongeza wajumbe kwa kuendesha mchakato kwa amani na ustaarabu

Anna Shinini kura 23

Scholar Molel 37

Paulina Nahato 71

Loema Peter 90

Joyclen Umbulla 168

Senorina Yunus 214

Rustina Rahh 703

Regina Ndege Qwaray 891

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button