GHANA : Matokeo ya uchaguzi wa rais yathibitishwa

GHANA : MATOKEO ya uchaguzi wa rais nchini Ghana yamethibitishwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo  na kumtangaza rasmi mshindi ambaye ni mgombea wa upinzani na rais wa zamani John Mahama.

Mahama alishinda kwa asilimia 56.6 dhidi ya asilimia 41.6 ya kura aliyopata Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia.

Wataalam wa masuala ya  siasa wanasema  ushindi huu ni mkubwa katika nchi hiyo kwa miaka 24.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini Ghana, Jean Mensa  amesema waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni asilimia 60.9. SOMA: Makamu wa rais Ghana kugombea urais

Mahama alisema,” nahisi kufurahishwa na uchaguzi huu watu wamepiga kura na kupata matokeo amzuri katika historia ya Ghana,” alisema  Mahama.

Aliongezea kuwa,” historia nyingine ni kumchagua makamu wa rais mwanamke hii ni hatua nyingine katika historia ya siasa ya  Ghana,” Alimalizia.

Habari Zifananazo

Back to top button