Sababu yatajwa matumizi ya visima virefu, vifupi Ushetu

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema Halmashauri ya Ushetu imekuwa ikitumia mtandao wa maji wa visima virefu na vifupi kwa muda mrefu kwenye maeneo karibu yote ni kutokana na kukosa chanzo cha maji cha uhakika.

Serikali ilikuwa ikitumia fedha nyingi kuchimba visima virefu na vifupi lakini chini hakuna maji yakutosha hivyo wakaona waje na mkakakati wa kuyavuta kutoka kwenye chanzo cha uhakika cha Ziwa Victoria.

Waziri Aweso aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua ujenzi wa mradi wa maji wa kisima kirefu katika kijiji cha Busenda kata ya Chona halmashauri hiyo huku akieleza mradi wa Maji Ziwa Victoria tayari tenda ya utekelezaji imekwisha tangazwa.

“Nataka niwatoe hofu mkandarasi atakaye tekeleza atatangazwa baada ya siku 30 hivyo mateso ya kuhangaika kutafuta maji Sasa yanaenda kuisha” alisema Waziri Aweso.

Aweso alisema kilio cha mbunge na diwani amekisikia huku akimuelekeza meneja wa wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) katika fedha zilizobaki

Habari Zifananazo

Back to top button