Mawasilisho ya tafiti 218 yakabidhiwa kwa watunga sera

DAR ES SALAAM: MAWASILISHO 218 ya tafiti mbalimbali za afya, zimewasilishwa kwa watunga sera ili kuona namna ya kuleta matokeo changa kwenye sekta ya afya.
Zoezi hilo limefanyika leo ikiwa ni siku ya pili ya Kongamano la 13 la Kisayansi lililondaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS ) mara baada ya jana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufunga kongamano hilo ambapo leo limefungwa.
Akizungumza leo wakati wa kulifunga kongamano hilo, Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema kwa kutambua magonjwa hayana mipika pia mapendekezo yameangalia na watafiti wengine.

“Haya mapendekezo yameangalia na watafiti wengine duniani kote, maana magonjwa hayana mipaka, sema tunatofauti labda ukanda, kiwango cha maendeleo na mifumo ya afya,” amesema Prof Kamuhabwa.
“Asilimia kubwa ya waliotoa mawasilisho na kuhudhuria ni vijana wakiwemo wanafunzi, hii ni habari njema kuhakikisha kunakuwa na muendelezo,” ameongeza Prof Kamuhabwa.
SOMA ZAIDI
Prof Kamuhabwa ametaja baadhi ya mawasilisho kuwa namna ya kujiandaa na majanga yanapotokea, tafiti ya afya ya mama na mtoto namna ya kuokoa maisha ya mtoto.
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Kongamano hilo, Raphael Sangeda amesema mazimio ya kongamano yataenda kufanyiwa kazi, ambapo kuna tafiti nyingi zimefanyika.

Amesema lengo ni kuona tafiti hizo zikienda kuwa na tija kwa wananchi katika sekta ya afya.
“Lengo tuwafikie wananchi na tafiti zetu ziweze kuwa na mabadiliko chanya kwenye afya ya jamii,” amesema.
Amesema kuna baadhi ya tafiti moja kwa moja zinaweza kufanya mabadiliko kwenye miongozo mbalimbali ya afya.

Bhoke Juma, mwanafunzi wa mwaka wa pili Kada Afya ya Sayansi ya Mazingira ametoa wito kwa wanafunzi wengine kujikita kwenye tafiti na uvumbuzi wa masuala mbalimbali.

“Nimejifunza kufanya tathmini ya hatari ‘risk assesment’ kwenye mazingira ikiwemo utunzaji wa mazingira,” amesema Bhoke.



