Mawasiri NATO kukutana Brussels

BRUSSELS: MAWAZIRI wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO, wanakutana mjini Brussels kuzungumzia usalama na vita vya Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atashiriki mkutano huo ambao huenda ukawa wa mwisho wa ngazi za juu kushiriki, kabla utawala wa rais Joe Biden kuondoka madarakani.

Miongoni mwa  ajenda muhimu kujadiliwa ni masuala ya kipaumbele katika ushirikiano wa kiusalama kati ya Marekani na Ulaya yatajadiliwa ikiwemo kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya  Urusi, lakini pia kuimarisha ushirikiano na washirika wa NATO wa kusini katika kanda ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, na Sahel.

Mkutano huo pia utajadili maandalizi ya mkutano ujao wa kilele utakaofanyika The Hague mwezi Juni. SOMA: Mpango wa Zelensky kutangazwa

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button