Mbarawa aagiza ununuzi wa boti kukabiliana uvuvi haramu

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kununua boti inayokwenda kasi ‘speed –boat’ kwa ajili kufanya shughuli za utafutaji na uokozi katika mwambao wa Bahari  ya Hindi  na kusimamia uvuvi haramu.

Akitoa agizo hilo leo jijini Arusha wakati wa ukaguzi wa mabanda mbalimbali kwenye mkutano wa 16 wa Mapitio  ya Pamoja ya Sekta ya Usafiri, Profesa Mbarawa amesisitiza uwepo wa boti hizo utawezesha mamlaka hiyo kufanya doria mbalimbali.

“Kweli mnafanya kazi nzuri lakini hamna boti zinazoenda spidi ili kusimamia usalama wa vyombo vya usafiri majini pamoja na uchafuzi wa mazingira ,nunueni boti ili kulinda usalama wa bahari”.

Advertisement

amesema

Mkurugenzi wa TASAC, Mohamed Salum amesema jukumu la shirika  hilo ni kuhakikisha katika mwambao wa bahari unalindwa ni lazima wasimamie na kudhibiti uvuvi haramu, matukio ya uhalifu au meli kupita pasipozingatia masharti ya usafirishaji ikiwemo uchafuzi wa mazingira.

Amesema taasisi hiyo inajiendesha na inauwezo wa kupanga bajeti yake hivyo gharama ya boti  moja ya kisasa inagharimu sh, bilioni 2 hadi sh,bilioni 10 ambapo boti hizo hubeba watu sita au wanane lakini zina uwezo wa kukimbia

“TASAC haina chombo chake yakitokea majanga lazima tuongee na wenzetu wa Kikosi cha Jeshi la Polisi Majini na Jeshi la Wananchi Tanzania Kikosi cha Wanamaji (NAVY) ili  waweze kudhibiti matukio mbalimbali ya baharini lakini tumejipanga mwaka ujao wa fedha tununue boti hizi kwaajili ya shughuli zetu za kulinda mwambao wa bahari “.

1 comments

Comments are closed.