Mbegu mpya 16 korosho, karanga zagunduliwa

DAR ES SALAAM; Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imegundua mbegu mpya 16 za mazao ya maharage, korosho na karanga zitakazoanza kutumika msimu wa kilimo mwaka 2024/2025.

Mbegu hizo mpya ambazo zimeidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu zimefanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zinasifa za kutoa mavuno mengi, kuwa na ukinzani dhidi ya magonjwa na kukomaa mapema.

Mbegu hizo ni pamoja na aina sita za maharage; TARIBEAN6, TARIBEAN 7, TARIBEAN 8, TARIBEAN 9, TARIBEAN 10, TARIBEAN 11 na karanga aina mbili ambazo ni TARIKA 1 na TARIKA 2.

Pia katika zao la korosho jumla ya aina nane za mbegu bora za Korosho zimegunduliwa ambazo ni TARIKO-1, TARIKO-2, TARIKO-3, TARIKO-4, TARIKO-5, TARIKO-6, TARIKO-7 na TARIKO- 8.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Mtaalam wa utafiti zao la karanga Dk Happy Daud, amesema mbegu za karanga zilizogunduliwa pamoja na sifa zingine ni za muda mfupi na hazishambuliwi na magonjwa tofauti na mbegu za muda mfupi zilizopo hushambuliwa na magonjwa ya majani.

Naye Mkuu wa Idara ya Ugunduzi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Korosho Kituo cha TARI Naliendele, Dadili Majune amesema mbegu hizo mpya zina ukinzani wa ugonjwa wa blaiti, uzaaji na ubora katika soko la kimataifa.

Majune amesema, ugunduzi huo utasaidia kupunguza matumizi ya viuatilifu vya ugonjwa wa blaiti katika zao la korosho.

Soma:  Mbegu za asili fiwi, ulezi hatarini kutoweka

Mratibu wa Maharage Kitaifa Reinfrid Maganga kutoka kituo cha TARI-Uyole, amesema mbegu sita za maharage zilizogunduliwa pamoja na kuwa na tija zaidi zina sifa nyingine, TARIBEAN 6 ni maharage lishe yenye madini ya zinki na chuma kwa wingi zaidi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button