Mbegu za asili kufanyiwa utafiti

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA), inakusanya mbegu za asili kwa ajili ya kuzihifadhi zisipotee, ikiwa ni pamoja na kuzifanyia tafiti.

Mkuu wa Kitengo cha Taifa cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea kutoka TPHPA, Mujuni Sospeter amesema hayo jijini Dodoma alipozungumza na mwandishi wetu wa HabariLeo

Amesema kutokana na tafiti wanazozifanya kwenye mbegu hizo za asili wamegundua zina sifa nyingi ambazo zinaweza zikatumika kwa ajili ya kuboresha aina ya mbegu ili ziweze kuwa bora zaidi.

“Kutokana na umuhimu huo serikali imeona ianzishe hii program ya kuhifadhi hizi mbegu za asili ili tuzitumie wakati tunapozihitaji kwa sasa lakini pia vizazi vinavyokuja vyote vije vizikute na wao wazitumie pale wanapozihitaji,” amesema.

Amesema mpaka sasa wameshakusanya takriban sampuli 10,000 toka wameanza kuzikusanya, malengo ikiwa ni kufikia sampuli 100,000.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by TPHPA (@tphpa_tz)

“Tunapozihifadhi hizi mbegu pia tunazifanyia tafiti za awali kujua tabia zake, sifa zake, ambapo hizo tabia na sifa zinasaidia kama msingi wa utafiti.

 SOMA: Sh bilioni 2 kuboresha huduma ukaguzi TPHPA

“Tunatambua kuwa aina zote za mbegu tunazikuta kwenye biashara au maduka ya pembejeo huwa zinakuwa na mahali zinaanzia, zinakuwa na msingi wa utafiti,” amesema.

Amesema kupitia mbegu za asili wanafanya utafiti ili kujua sifa zake za awali,uwezo wake na baada ya kujua inawasaidia kuweza kushirikiana na taasisi nyingine za utafiti kwa lengo la kuzalisha mbegu bora zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button