Mbowe aomba saa 48 kutoa msimamo Chadema

DAR ES SALAAM; MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewaomba viongozi, wanachama na makada waliofika nyumbani kwake wampe saa 48 za kutafakari ombi lao la kumtaka kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam , Mbowe amewaeleza kuwa hataingia kwenye vita itakayokibomoa chama hicho bali ataingia kwenye vita itakayokijenga.
“Nimesikia ombi lenu, nawaomba mnipe saa 48 za kutafakari kisha nitazungumza na wahariri wa vyombo vya habari Jumamosi (Desemba 21, 2024) hapahapa nyumbani kutoa msimamo wangu.
“Ninachowaahidi kuwa sitaingia kwenye vita itakayopasua chama, nitaingia kwenye vita itakayokijenga chama chetu. Kuanzia sasa hadi Jumamosi nitakuwa nafuatilia kwa karibu mambo yanavyokwenda, nikiona chama kinakwenda shimoni, Kamanda nitaingia mzigoni,” amesema Mbowe.

“Nimekuwa na wakati mgumu na familia yangu. Hakuna kipindi familia yangu imenikalia mguu pande kama kipindi hiki, wananiambia ‘baba inatosha, toka achana na siasa rudi nyumbani uendelee na maisha mengine’. Sasa familia yangu nayo ina nguvu katika maisha yangu, lakini vilevile na familia ya Chadema nayo ina nguvu sasa, ” amesema Mbowe na kuongeza:
“Nimekuwa na wakati mgumu na familia yangu. Hakuna kipindi familia yangu imenikalia mguu pande kama kipindi hiki, wananiambia ‘baba inatosha, toka achana na siasa rudi nyumbani uendelee na maisha mengine.
“Sasa familia yangu nayo ina nguvu katika maisha yangu, lakini vilevile na familia ya Chadema nayo ina nguvu sasa.”
“Chadema inaongozwa kwa vikao, sio matamko, hivyo anavyotoka kiongozi mwenzetu na kusema kitu cha tofauti lazima tumuhoji.
“Juzi nilipata ujumbe kwa viongozi wa mikoa wana jambo lao wangependa kunitembelea, waliniomba kibali cha kunitembelea, nikawadadisi mnakuja kufanya nini.
“Nikawauliza mnakuja watu wangapi, wakaniambia kadhaaa, jana wakasomba viti na mahema. Waliambia nisitokea ndani hadi waniambie nimekuwa mwali, ambaye nimetoka sasa,” amesema Mbowe



