MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa chama chake kitaendelea kuishughulikia serikali na pia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbowe ameyasema hayo leo Machi 8, 2023 katika kongamano maalum la wanawake wa Chadema ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Amesema Napenda kusisitiza, sisi tutaendele kuishughulikia serikali yako kikamilifu, na chama chako kikamilifu, na kutekeleza majukumu yetu kama wapinzani, kukishughulikia chama chako bila hofu, ila tutafanya yale yaliyo na uhakika, ili si tu muweze kuinyoosha nchi, ila na sisi tupate nafasi ya kuongoza siku za usoni.”Amesema Mbowe na kuongeza
“Mheshimiwa Rais, Demokrasia haipaswi kuwa chaguo yaani ‘option’, hakuna taifa lililopuuza demokrasia, likakumbatia mifumo ya udikteta na uonevu likastawi, tunapaswa kukumbatia mifumo yenye hofu ya Mungu.
“Tunataka viongozi wapatikane katika chaguzi za haki na hapo tutapata kusema kiongozi wetu kuwa ni chaguo la Mungu, tutajiepusha na laana.
” Amesema Mbowe
Aidha, Mbowe amesema Chadema ipo tayari kusamehe na kusahau, kwa sababu Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati ya kuliunganisha taifa, kuponya majeraha kwa roho yake nyeupe na uwazi.
“Katika mazingira ya kawaida, serikali na chama chako kingepaswa kuliomba radhi taifa kwa tuliyopitia. Angalieni mfano wa NAC pale mtawala anapotoka kwenye mstari wanamng’oa hata akiwa madarakani nyie mnakumbatiana na kulinda.
“Bahati leo kaingia mama mwenye roho nyepesi, roho nyeupe hadi sisi wengine tunamshangaa, hii roho ya kutuunanisha watanzania wote inapaswa kulindwa kwa kuwekwa kwenye katiba ili asije mwingine akaturudisha tulipotoka.” Amesema Mbowe