Mbunge ataka punguzo la kodi vifaa vya mazoezi

MBUNGE wa Viti Maalum, Sylvia Sigula amehoji bungeni kama serikali haioni haja ya kupunguza kodi kwenye vifaa vya mazoezi kwa kuwa mazoezi ni tiba.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande amesema: “Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mwaka 2014, kama ilivyofanyiwa marekebisho mbalimbali, imeainisha msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika kipengele cha 6(1) na jedwali la misamaha lililopo kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148.

“Bidhaa au huduma zilizopewa msamaha wa Kodi ya VAT ni pamoja na vifaa vinavyotumiwa kwa ajili ya tiba. Msamaha kwenye vifaa tiba vya mazoezi yaani physiotherapy hutolewa kwa hosiptali zilizosajiliwa na kuidhinishwa na Waziri wa Afya, ambapo hupatiwa msamaha wa kodi kwa lengo la kuboresha afya kupitia mazoezi, ambayo ni njia bora ya kuzuia magonjwa na kuboresha ustawi wa jumla wa jamii,” amesema Naibu Waziri Chande.

Habari Zifananazo

Back to top button