Mbunge Biharamulo atoa sadaka ya futari

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesa amekabidhi vyakula mbalimbali kwa shekhe wa Wilaya ya Biharamulo ikiwa ni sehemu ya kuwafutulisha waislamu wenye uhitaji katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi maharage, mchele, ngano, unga wa sembe, mafuta ya kula na Sukari amesema kuwa umekuwa utamaduni wake wa kuwashika mkono waislamu wote Wilaya ya Biharamulo kwa kutoa futari ambayo anaamini inasaidia kwa namna moja ama nyingine wahitaji wanaoendelea na mfungo watakaopata.

Aidha amewaomba waislam wote kuendelea na mfungo wa Ramadhani na futari hiyo kupitia shehe wa wilaya itaweza kuwafikia walengwa kupitia utaratibu watakaojipangia kugawa kwa walengwa.

“Tuendelee kufunga na kuliombea taifa letu amani ,naamini haya mahitaji ya chakula yatawafikia walengwa na  kusaidia hasa wale wasio na uhitaji,Mimi kama kawaida yangu Niko na ninyi katika mfungo huu ambao unamuweka Kila mtu karibu na Mungu,”amesema Chiwelesa.

Kwa upande wake shehe wa Wilaya ya Biharamulo Hamza khatib amemshukuru Mbunge kwa swadaka aliyoitoa katika kipindi Cha Ramadhani kwani umekuwa utamaduni wake  tangu mwaka 2021 na kuhusu swadaka yenyewe amesema itawafikia walengwa kwa utaratibu waliojiwekea ili iweze Kusaidia wahitaji.

Hata hivyo katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Biharamulo Adam Sudi amesema swadaka aliyotoa Mbunge ni moyo wake wa upendo kwa waislamu wote licha ya yeye kuwa dhehebu tofauti lakini amekuwa kiungo muhimu kufutukisha waislam Kila mfungo wa Ramadhani.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button