HALMASHAURI ya Wilaya ya Ngorongoro imenunua jumla ya dozi 44,000 za chanjo kwa ajili ya kuchanja mbuzi na kondoo ili kudhibiti ugonjwa wa homa ya mapafu (CPPP) kutoka kwa Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania Kanda ya Kaskazini (TVLA).
Hayo yamesemwa wilayani Ngorongoro na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Murtallah Mbillu, wakati wa makabith amepokea jumla ya dozi 44,000 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Mbuzi (CPPP) kutoka Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania.
Mbillu amesema lengo la serikali ni kuimarisha afya za mifugo na kuboresha uchumi wa wananchi wa Ngorongoro, ambao asilimia 80 ni wafugaji huku Wilaya hiyo ikiwa na mifugo mingi zaidi
“Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imenunua jumla ya dozi 44,000 za chanjo kwa ajili ya kuchanja mbuzi na kondoo ili kudhibiti ugonjwa wa Homa ya mapafu ya mbuzi na kondoo kutoka Wakala ya Maabara ya Tanzania,”
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania Kanda ya Kaskazini (TVLA) Dk,Lowenya Mushi, amesema lengo la ni kuhamasisha wananchi kuchanja mifugo yao ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo ambao umekuwa changamoto kwa muda mrefu.
Huku Diwani wa Kata ya Oloipiri, Lucas Krusas, ameishukuru serikali ya kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kudhibiti ugonjwa wa homa ya mapafu kwa mifugo kwani ni hatua muhimu kwa wafugaji.