Mbwana Samatta arejeshwa Stars
WACHEZAJI 23 wa kikosi cha timu ya taifa-Taifa Stars- wameitwa kuingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Taifa Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya DR Congo ugenini Oktoba 10 kabla ya kurudiana Dar es Salaam Oktoba 15.
SOMA: Nahodha Taifa Stars amsifu Samia
Wachezaji walioitwa ni Ally Salim, Zuberi Foba, Yona Amos, Mohamed Hussein, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Ibrahim Hamad, Bakari Nondo, Dickson Job, Abdulrazak Hamza, Haji Mnoga, Adolf Mtasingwa, Habib Khalid na Himid Mao.
Wengine ni Mudathir Yahya, Feisal Salim, Suleiman Mwalim, Cyprian Kachwele, Clement Mzize, Mbwana Samatta, Kibu Dennis, Nasoro Saadun na Abdullah Said.
Stars inayonolewa na kocha Hemed Suleiman ipo kundi H ikishika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 2.
DR Congo inaongoza kundi hilo ikikusanya pointi 3 huku Ethiopia ikiwa ya 3 na pointi yake 1 wakati Guinea ni ya mwisho haina pointi.