Mchengerwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Busega

DODOMA:Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu Veronica Sayore kuanzia Septemba 22, 2023 ili kupisha uchunguzi.

Uamuzi huo wa Mchengerwa unakuja baada ya kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhisha, kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mchengerwa amemwelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuunda timu ya uchunguzi na mwenendo wa utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo pamoja na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Katika hatua nyingingine Waziri Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia dhana ya ushirikishwaji wa viongozi, watendaji na wanannchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button