Mchezaji gofu ashinda mil 6.8/- mashindano Gymkhana

Mashindano ya Gofu kwa ajili ya kumuenzi mchezaji wa zamanı wa timu ya taifa ya wanawake ya gofu, marehemu Lina Nkya msimu wa nne yamezidi kuchanja mbuga huku mchezaji wa wakulipwa kutoka klabu ya gofu Gymkhana Dar es Salaam, Fadhil Nkuya akiibuka tena mshindi wa kwanza na kujipatia kitita cha Sh milioni 6.8.
Michuano hiyo ambayo ilifanyika katika katika Viwanja vya Lugalo Gofu jijini Dar es Saaalm kuanzia Julai 17 hadi 20, 2025 iliwakutanisha wachezaji zaidi ya 150 na Nkya amezidi kuonesha umwamba wake kwa upande wa wachezaji wa gofu wa kulipwa na kufanya kushika nafasi hiyo kwa mara ya sita mfululizo.
Akizungumza mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo kwa upande wa wachezaji wa kulipwa, Nkya amesema amekuwa mshindi wa mashindano hayo mara ya sita mfululizo na kwamba siri kubwa ya mafanikio yake ni mazoezi bila kuchoka wala kukata tamaa.



