Mchungaji afurahishwa kampeini ya kisheria kufika kanisani

MCHUNGAJI Wilson Wilibadi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini Magharibi KKKT mtaa wa Mshasha kata Mshasha wilayani Missenyi amesema  ataungana na waumini wake kuiunga mkono kwa vitendo kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia.

Aliyasema hayo mara baada ya timu ya wataalamu wanaoratibu kampeni hiyo katika wilaya hiyo kuungana na waumini wa kanisa hilo kutoa elimu na ufafanuzi wa kisheria juu ya maswala mbalimbali yanayohusu sheria na jinsi ya kuyatatua

Mratibu wa kampeini hiyo Maximilian Fransis aliongoza timu ya kampeini hiyo kutoa elimu juu ya kuandika wosia kisheria, mirathi, ukatili, ardhi mambo mengi juu ya maswala ya sheria huku waumini wakipewa nafasi ya kuuliza maswali ya kuwasilisha changamoto zao zinazowakabiri hasa katika maswala ya sheria ili zitatuliwe.

Mchungaji wa kanisa hilo alisema ameifatilia kampeini hiyo kupitia vyombo vya habari nchini na anapongeza ubunifu wa Serikali ya Mama Samia kwa kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao hasa matatizo yao makubwa ni upungufu wa sheria na kuwapa elimu hiyo wanayoipata kupitia kwa wataalamu wa sheria anaamini itawasaidia kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Alisema kwa jinsi alivyofurahiswa na mafunzo ya kisheria anatizamia kuandaa kongamano kubwa la wanawake wa kanisa hilo na kuwaalika timu hiyo ili itoe mafunzo kwa wanawake wa kanisa hilo kuhusu haki zao kisheria ,jinsi ya kulimili ardhi ,jinsi ya kupata mali zao hasa wajane na jinsi ya kukomesha ukatili kwani anaamini wanawake ndio waathirika wakubwa wa maswala ya ukatili kwa kila kitu.

“Ni neema kubwa elimu hii imetufikia hadi kanisani ,kweli serikali haina ubaguzi hata Mimi nimejifunza mambo makubwa ambayo nilikuwa siyaelewi nimepata ufahamu wa kutosha ,wataalamu waliotumwa wamepikwa na kupikika ,nimefurahishwa sana na Mungu ampe nguvu Rais wetu ili aendelee kuwa mbunifu,” alisema Wilibadi

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo ambaye ni mlezi wa mitaa ya washirika Winifirida Gabriel aliipongeza kampeni hiyo kutolewa kwa uwazi na kutoa nafasi ya wananchi kuuliza maswali na kujibiwa.

Aliomba kampeini hiyo kuendelea kuwa endelevu hata ngazi ya vitongoji ili kupunguza kero na upotevu wa muda wa kupanga foleni mahakani na kudai kuwa kama wananchi watazijua vizuri sheria watapunguza kuzivunja na kujiletea maendeleo .

Tangu kampieni hiyo kuzinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro mkoani Kagera Aprili 14 mpaka sasa wilaya ya Missenyi kata 15 zimefikiwa vijiji 45 na wananchi wametatuliwa changamotoo zao za kisheria na kujengewa uelewa katika maswala ya Ardhi, ndoa, mirathi ,ukatili,matunzo na madai .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button