Mechi tatu za maamuzi, vita ya Ligi Kuu

DAR ES SALAAM; Ligi ya Championship kwasasa ipo katika hesabu kali kila timu inajitafuta kupata hesabu kamili ifikapo mwishoni mwa msimu.
Imesalia michezo mitatu kwa kila timu ili kujua timu zipi zitapanda moja kwa moja Ligi Kuu msimu ujao na zitakazocheza hatua ya mtoano kuisaka nafasi ya Ligi Kuu lakini pia ni zipi zitashuka daraja.
Timu ya KenGold kutoka Mbeya ipo katika mazingira mazuri ya kupanda Ligi kuu ambapo mpaka sasa wanaongoza usukani wa ligi hiyo wakiwa na alama 61, Pamba ya Mwanza nao hawapo nyuma kuna nyota njema kwao, huenda safari hii wakaipata tiketi ya kupanda msimu ujao mpaka sasa wapo nafasi ya pili na alama 58.
Wanajeshi wa Mpakani Biashara United ya Mara wakichanga vyema karata zao kuna uwezekano wa kurejea Ligi Kuu msimu ujao wanakamata nafasi ya tatu wakiwa na alama 56.
Tumekuwekea msimamo na ratiba ya michezo iliyosalia kwa timu zote katika ligi hiyo.
 
 

Habari Zifananazo

Back to top button