Merino akamilisha vipimo Arsenal

KIUNGO Mikel Merino amekamilisha vipimo vya afya tayari kwa kujiunga na klabu ya Arsenal ya England akitokea Real Sociedad

Taarifa iliyotolewa na mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano, klabu hizo mbili zinabadilishana nyaraka za mikataba kukamilisha uhamisho huo.

SOMA: Arsenal yaitangulia Juve kuwania saini ya Calafiori

Merino anajiunga na Arsenal kwa dau la pauni milioni 32 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 5 (Add-ons).

Kiungo huyo raia wa Hispania atasaini mkataba wa miaka minne wenye kipengele cha kuongeza mkataba mwingine.

SOMA: Tomiyasu yupo sana Arsenal

Habari Zifananazo

Back to top button