Merz: Tunakwenda Gaza kutafuta majibu

BERLIN, UJERUMANI : UJERUMANI , Ufaransa na Uingereza zinapanga kuwatuma mawaziri wao wa mambo ya nje katika Ukanda wa Gaza wiki ijayo, ikiwa ni juhudi za kushinikiza hatua za haraka kukabiliana na hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa na Mfalme wa Jordan, Abdullah II, mjini Berlin. SOMA: Malori 120 ya msaada yaingia Gaza

Merz amesema nchi hizo zinaamini kuwa ni wakati muafaka kwa serikali ya Israel kutambua kuwa hali ya Gaza inahitaji hatua za haraka, hasa katika kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia kwa urahisi. Aidha, amesema ziara hiyo inalenga pia kuimarisha juhudi za kidiplomasia kwa ajili ya kupunguza mateso ya raia wa kawaida wa Palestina.

Kwa muda mrefu, Ujerumani imekuwa mshirika wa karibu wa Israel, lakini pamoja na Ufaransa na Uingereza, sasa imeongeza sauti katika kuitaka Israel kuruhusu misaada ya kibinadamu Gaza. Wiki iliyopita, nchi hizo tatu zilisaini taarifa ya pamoja zikishinikiza suluhisho la kudumu la changamoto za misaada na huduma za msingi katika Ukanda huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button