Mgombea ujumbe NEC arudisha fomu Arusha

MFANYABIASHARA Maarufu Jijini Arusha, Richard Poul maarufu Marcas amajitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi Moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa Arusha akisema kuwa lengo lake ni kuwaunganisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kitu kimoja.

Marca alisema na kuwataka wajumbe wa uchaguzi kuangalia sifa za mgombea na kuacha mara moja kuchagua mgombea kwa rushwa kwani rushwa kwake ni adui wa haki na kamwe hawezi kufanya hivyo kwani anajiamini kuwa anatosha.

Alisema na kusisitiza kuwa uchaguzi huo wa marudio uligubikwa na rushwa na ndio maana viongozi wa juu wa CCM Tiafa waliufuta kw amaslahi ya chama hivyo basi wajumbe wa Uchaguzi wasirudie tena makosa hayo kwani ni kuendelea kukidhallisha chama kwa tama za watu wachache.

Naye Silanka Mollel yeye alisema kuwa yeye ana sifa za kutosha kuchaguliwa kuwa MNEC Mkoa wa Arusha kwa kuwa alishawahi kushika nafasi mbali mbali za chama hivyo haoni sababu ya wajumbe wa uchaguzi kutokumchagua.

Mollel na lisema na kusisistiza kuwa malengo makubwa akichaguliwa ni kuwaunganisha wana CCM wote Mkoani Arusha kuwa kitu kimoja na kuwa na mshikamano wa dhati kwa maslahi ya chama na sio vinginevyo.

Habari Zifananazo

Back to top button