Mgombea urais CUF atangaza vita wezi mali za umma

DAR ES SALAAM: MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo, amesema iwapo atachaguliwa serikali yake itakuwa na msimamo mkali dhidi ya wezi wa mali za umma.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Daily News Digital na kueleza kuwa katika kukomesha wizi wa mali za umma atahakikisha hakutakuwa na mchakato mrefu wa uchunguzi wa upotevu wa mali hizo, bali njia zilizotumika kuiba ndio zitakazotumika kuzirejesha.
Amesema wizi wa mali za umma unaendelea kutokana na uwepo wa mchakato mrefu wa uchunguzi, lakini pia adhabu zinazotolewa ni za kawaida jambo linalowafanya kuendelea na vitendo hivyo vya uhalifu.
“Sehemu kama Tanzania kuna wezi na sheria zinasema mwizi lazima achunguzwe, kwa hiyo kwa sheria hizi mwizi wa Tanzania ni ngumu sana kumfukuza.
“Ukumbuke kwamba mwizi wa mali za umma akiiba adhabu huwa ni tatu kuna adhabu ya kupewa barua ya onyo, kupunguziwa mshahara na kufukuzwa kazi, lakini hawazungumzii habari ya pesa iliyopotea inarudije, hivyo msimamo wa CUF ni kwamba pesa ilipotokea ndio itakaporudia hakuna mambo ya uchunguzi,” amesema Gombo na kuongeza:
“Pesa ya serikali inajulikana imeingia imeingia kwa nani na imechukuliwa na nanim na wezi serikalini wanajulikana lakini sheria haiwapi nafasi ya kuridisha hizo pesa”
Amesema ndani ya siku 100 za kwanza madarakani atashirikiana na wadau wote kushauriana namna ya kuboresha sheria zitakazowawajibisha wezi wa mali za umma.
“Lazima tukubaliane huyo mwizi tunamfukuza kazi au tunampeleka mapumzikoni Dubai aende Dubai tumnunulie na nyumba tumwambie tumekuelewa bwana ukiiba tunakupa gari uende kabisa lakini watu wakisema akiiba huyu tumtandike viboko, tutamtandika si wananchi wamesema kwa sababu mali aliyoiba ni za wananchi sio za Gombo,” amesema mgombea huyo.
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
Google paid $220 an hour on the internet. My close relative has been without labor for nine months and the earlier month her compensation check was 25k by working at home for 10 hours a day….. Everybody must try this job now by just use this link
COPY THIS→→→→ http://Www.CartBlinks.Com