Mhagama kuzikwa Des.16 kijijini Ruanda

DODOMA; MBUNGE wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama aliyefariki dunia leo Desemba 11, 2025 mjini Dodoma, atazikwa Desemba 16, 2025 Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge usiku huu, inaonesha kesho Desemba 12, 2025 mwili utawasili nyumbani kwa marehemu eneo la Itega, Dodoma ambapo maombolezo yatakuwa yakiendelea.

Ratiba inaonesha Jumamosi Desemba 13, kutakuwa na Ibada kwenye Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege, Dodoma, ambapo pia salamu za rambirambi zitatolewa na pia wananchi watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu na baadaye alasiri safari ya kuelekea Songea itaanza.

Desemba 14 mwili utapelekwa Kanisa Katoliki Matogoro, Songea Mjini ambako kutakuwa na ibada, kisha baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwa marehemu Makambi, Songea Mjini.

Jumatatu Desemba 15 asubuhi safari ya kuelekea Peramiho , ambapo kutafanyika ibada , salamu za rambirambi na kuaga mwili, kabla ya siku inayoafuata kuelekea kijijini Ruanda, wilayani Mbinga kwa maziko.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button