Mhandisi TANROAD awabwaga wanne Bukoba Mjini

BUKOBA: Mhandisi wa TANROAD, Johnston Mtasingwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 1,408 na kuwabwaga wenzake zaidi ya wanne waliokuwa walishiriki mchakato wa kumpata Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Bukoba Mjini
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Bukoba Mjini, Shabani Mdohe ametangaza kura za maoni ambapo amewataja wengine waliogombea kuwa ni Alex Denis Kura 804 , Almasoud Kalumuna kura 640 Jamila Hassan kura 66 na Koku Rutha kura 44
Alisema kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 3033 waliojitokeza kupiga kura ni 2978 zilizoharibika ni kura 20 na kura halali ni 2958.


