“CHINI ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kila sehemu kuna alama ya maendeleo yaliyofanywa na utawala wake kuanzia shule, zahanati, barabara, miradi ya maji na kadhalika. Tuna kila sababu ya kujivunia uongozi wake. Kwa kweli amefanya na anaendelea kufanya makubwa,” anasema Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Rorya, Loth Lemeirut.
Kada huyo wa CCM anasema mbali na kuimarisha umoja wa nchi kwa kuleta maridhiano ya kisiasa, Samia amegusa karibu kila nyanja inayohusu maendeleo ya mwananchi. Kwa upande wa barabara, Lemeirut ambaye alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda kabla ya kuhamishiwa Rorya hivi karibuni, anasema ameshuhudia miradi mikubwa ya barabara ikitekelezwa kwa fedha za tozo ya mafuta na fedha za jimbo na hivyo maeneo mengi kufunguka.
“Nitazungumzia zaidi Wilaya ya Bunda ambayo ndiyo naweza kusema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia nilikuwa nafanya kazi. Takribani sasa wilaya yote imefunguka kwa kuwa na barabara za uhakika zinazoweza kupitika katika vipindi vyote vya misimu ya mvua na jua kwa mwaka.
” Anasema mtu aliyetoka Bunda miaka miwili iliyopita, akirudi leo atashangaa kuona barabara zinapitika karibu kila kata huku miradi mingine ya barabara kwa kata chache zilizobaki ikiendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa. Franco Nyamegeko (40), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Bunda anaipongeza serikali kupitia Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) kwa namna ilivyoifungua wilaya hiyo kwa barabara. Bunda ipo kando ya Ziwa Victoria.
“Mimi ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya na kwa kweli ninatembea kifua mbele kuona Ilani tuliyoinadi kwa wananchi ya mwaka 2020 –2025 inatekelezwa kwa kishindo kiasi hiki. Ama kwa hakika ni jambo la kufurahisha sana.
“Naweza kusema katika wilaya yetu ya Bunda hakuna diwani anayelalamika kuhusu miundombinu ya barabara zaidi ya kumshukuru Rais Samia (Suluhu Hassan) kwa kazi iliyotukuka,” anasema. Kada huyo wa CCM anampongeza kwa dhati Meneja wa Tarura Wilaya ya Bunda, Baraka Mkuya kwa kazi kubwa na usimamizi madhubuti wa ujenzi wa barabara wilayani humo. wananchi wangu walikuwa wanapata shida kutokana na barabara hii kutopitika hasa ‘Miaka 2 ya Samia kila kata Mara inapitika kwa barabara’ wakati wa masika,” anasema Manumbu.
Anasema barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha kata nne za Iramba, Chitengule, Namuhura na Neruma ambazo wananchi wake wanajihusisha na kilimo na uvuvi. Meneja wa Tarura Wilaya ya Bunda, Mkuya, anasema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia, Tarura wilayani humo iliidhinishiwa bajeti ya zaidi ya Sh bilioni 11 walizotumika kwenye ufunguzi wa barabara za urefu wa kilometa 48.7 ambazo hazikuwepo kabisa na kutengeneza barabara za udongo za urefu wa kilometa 368.164.
Fedha hizo pia anasema zinatengeneza Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kwa barabara. Hapa akifungua barabara ya Nyahua-Chaya ya urefu wa kilometa 85.4 mkoani Tabora mwaka jana. MAKALA barabara kwa kiwango cha changarawe za urefu kilometa 228.47, zimejenga madaraja makubwa tisa, vivuko 192 na ujenzi wa mitaro ya maji ya urefu wa mita 19,727.
Kwa upande wake, Meneja wa Tarura Wilaya ya Tarime, Charles Marwa anasema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia, wilaya iliidhinishiwa zaidi ya Sh bilioni 10 kwa ajili ya kufungua, kujenga na kukarabati barabara ili kuifanya Tarime kufunguka zaidi.
Anafafanua kwamba kiasi hicho kililenga ujenzi wa barabara za urefu wa kilometa 111.63 ambazo hazikuwepo kwa maana kwamba yalikuwa mapori, ujenzi wa barabara za udongo kilometa 577.54 na barabara kwa kiwango cha changarawe kilometa 71.5. Pia fedha hizo anasema ni kwa ajili ya ujenzi wa madaraja makubwa mawili, ujenzi wa madaraja madogo (vivuko) 102 na ujenzi wa mitaro ya maji ya urefu wa mita 2,336.
“Kwa kweli tunamshukuru Mheshimiwa Rais wetu Samia kwa kutupatia fedha hizi na kwa sasa Wilaya ya Tarime takribani kila mahali kunapitika, milima imekatwa ambapo tangu kuumbwa kwa dunia hakukuwahi kuwepo na barabara katika baadhi ya maeneo haya ya milimani. Ni maeneo ambayo wananchi walidhani isingewezekana kupatikana barabara lakini kwa sasa tumetengeneza barabara ambayo inapitika vizuri tu,” anasema Marwa.
Kwa upande wake, Hussein Abbas, Meneja wa Tarura Wilaya ya Rorya anasema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia, Tarura wilayani Rorya waliidhinishiwa zaidi ya Sh bilioni 7 kwa ajili ya kuanzisha barabara ambazo hazikuwepo za urefu wa kilometa 37, barabara za udongo kilometa 224 na kujenga au kukarabati barabara kwa kiwango cha changarawe kilometa 64, madaraja makubwa sita, ujenzi wa vivuko 79 na ujenzi wa mitaro ya maji ya urefu wa mita 1,900.
“Kwa kweli Rorya kwa sasa inapitika maana hapo awali ilikuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya maeneo kutoa mazao shambani kuyapeleka sokoni,” anasema Abbas. Joseph Mkwizu, Meneja wa Tarura Wilaya ya Musoma anasema wilaya hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia ilipatiwa Sh bilioni 15 na serikali, fedha ambazo zimetumika kwa kuanzisha barabara ambazo hazikuwepo za kilometa 87.69.
Pia zimetumika kutengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe za urefu wa kilometa 282.94, ujenzi wa madaraja makubwa 17, madaraja madogo (vivuko) 334 na ujenzi wa mitaro ya urefu wa mita 15,700. Meneja wa Tarura Mkoa wa Mara, Boniface Magani anasema katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia mkoa umezidi kufunguka kwa barabara kutokana na serikali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi au ukarabati wa barabara na madaraja.
“Sisi wakazi wa Mara tunampongeza Rais wetu Samia na serikali yake kwani amefanya kazi kubwa kutuongezea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya barabara katika wilaya zote za Mkoa wa Mara. “Kwa sasa lawama kutoka kwenye mabaraza ya madiwani zimepungua kama si kuisha kabisa na wananchi wana furaha kwani kata zote zinapitika kutokana na kazi ya kujenga barabara tulioufanya,” anasema. Magani anasema sehemu nyingi wamebadili barabara za udongo kuwa za changarawe na kujenga vivuko vikubwa na vidogo mbali na kuanzisha barabara ambazo hazikuwepo kabisa
“ CHINI ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kila sehemu kuna alama ya maendeleo yaliyofanywa na utawala wake kuanzia shule, zahanati, barabara, miradi ya maji na kadhalika. Tuna kila sababu ya kujivunia uongozi wake. Kwa kweli amefanya na anaendelea kufanya makubwa,” anasema Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Rorya, Loth Lemeirut.
Kada huyo wa CCM anasema mbali na kuimarisha umoja wa nchi kwa kuleta maridhiano ya kisiasa, Samia amegusa karibu kila nyanja inayohusu maendeleo ya mwananchi. Kwa upande wa barabara, Lemeirut ambaye alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda kabla ya kuhamishiwa Rorya hivi karibuni, anasema ameshuhudia miradi mikubwa ya barabara ikitekelezwa kwa fedha za tozo ya mafuta na fedha za jimbo na hivyo maeneo mengi kufunguka.
“Nitazungumzia zaidi Wilaya ya Bunda ambayo ndiyo naweza kusema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia nilikuwa nafanya kazi. Takribani sasa wilaya yote imefunguka kwa kuwa na barabara za uhakika zinazoweza kupitika katika vipindi vyote vya misimu ya mvua na jua kwa mwaka.” Anasema mtu aliyetoka Bunda miaka miwili iliyopita, akirudi leo atashangaa kuona barabara zinapitika karibu kila kata huku miradi mingine ya barabara kwa kata chache zilizobaki ikiendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa. Franco Nyamegeko (40), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Bunda anaipongeza serikali kupitia Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) kwa namna ilivyoifungua wilaya hiyo kwa barabara. Bunda ipo kando ya Ziwa Victoria.
“Mimi ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya na kwa kweli ninatembea kifua mbele kuona Ilani tuliyoinadi kwa wananchi ya mwaka 2020 –2025 inatekelezwa kwa kishindo kiasi hiki. Ama kwa hakika ni jambo la kufurahisha sana. “Naweza kusema katika wilaya yetu ya Bunda hakuna diwani anayelalamika kuhusu miundombinu ya barabara zaidi ya kumshukuru Rais Samia (Suluhu Hassan) kwa kazi iliyotukuka,” anasema. Kada huyo wa CCM anampongeza kwa dhati Meneja wa Tarura Wilaya ya Bunda, Baraka Mkuya kwa kazi kubwa na usimamizi madhubuti wa ujenzi wa barabara wilayani humo.
wananchi wangu walikuwa wanapata shida kutokana na barabara hii kutopitika hasa ‘Miaka 2 ya Samia kila kata Mara inapitika kwa barabara’ wakati wa masika,” anasema Manumbu. Anasema barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha kata nne za Iramba, Chitengule, Namuhura na Neruma ambazo wananchi wake wanajihusisha na kilimo na uvuvi.
Meneja wa Tarura Wilaya ya Bunda, Mkuya, anasema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia, Tarura wilayani humo iliidhinishiwa bajeti ya zaidi ya Sh bilioni 11 walizotumika kwenye ufunguzi wa barabara za urefu wa kilometa 48.7 ambazo hazikuwepo kabisa na kutengeneza barabara za udongo za urefu wa kilometa 368.164. Fedha hizo pia anasema zinatengeneza Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kwa barabara. Hapa akifungua barabara ya Nyahua-Chaya ya urefu wa kilometa 85.4 mkoani Tabora mwaka jana.
MAKALA barabara kwa kiwango cha changarawe za urefu kilometa 228.47, zimejenga madaraja makubwa tisa, vivuko 192 na ujenzi wa mitaro ya maji ya urefu wa mita 19,727. Kwa upande wake, Meneja wa Tarura Wilaya ya Tarime, Charles Marwa anasema kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia, wilaya iliidhinishiwa zaidi ya Sh bilioni 10 kwa ajili ya kufungua, kujenga na kukarabati barabara ili kuifanya Tarime kufunguka zaidi.