WANAWAKE 263 wamepoteza maisha kutokana na uzazi katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2021, huku sababu nne zikielezwa kuchangia vifo hivyo.
Akizungumza bungeni Dodoma leo Novemba Mosi,2022, Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema vifo hivyo vimetokana na sababu nne, ambazo ni dawa za ganzi, upasuaji wakati wa kutolewa mtoto tumboni, tatizo la damu kuganda na maambukizi ya bakteria baada ya upasuaji.
Amesema ufuatiliaji uliofanywa na serikali umebaini kuwa kwa mwaka 2018, vifo vilivyosababishwa na dawa za ganzi na upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni ni 53 sawa na asilimia 3.
Amesema mwaka 2019 kulikuwana vifo 80 yaani asilimia 4.8 mwaka 2020 kulikuwa na vifo 65 swa na asilimia 4, mwaka 2021 kulikuwa na vifo 65 sawa na asilimia 4.5
“Wizara inashirikiana na vyama vya kitaaluma kutekeleza mkakati kwa kuwajengea uwezo watumishi wa vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi za zahanati, hadi hospitali za taifa katika eneo la utoaji ganzi na upasuaji kwa usalama kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya,” amesema.