Miaka 60 ya Mkoa wa Singida

Singida inasifika kwa lipi?

SINGIDA: Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi Oktoba 15, 1963 ambapo kabla ya hapo ulikuwa ni Wilaya ya Jimbo la Kati (Central Province) uliojumuisha Mkoa wa Dodoma.
Mkoa wa Singida uko katikati ya Tanzania, kati ya Longitudo 33027’5’’ na 35026’0’’ mashariki ya Greenwich, na kati ya latitudo 3052’ na 7034’ Kusini mwa Ikweta.
Singida inapakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kaskazini, Mkoa wa Dodoma upande wa Mashariki, Mikoa ya Mbeya na Iringa upande wa Kusini na Mikoa ya Tabora na Simiyu upande wa Magharibi.
Mkoa wa Singida una Wilaya 5 ambazo ni Singida, Iramba, Manyoni, Mkalama na Ikungi; zenye Halmashauri 7 za Singida, Singida Manispaa, Iramba, Manyoni, Mkalama, Ikungi na Itigi. Aidha Mkoa una Tarafa 21, kata 136, Vijiji 442, vitongoji 2,309 na majimbo ya uchaguzi 8.
Ukubwa wa eneo la Mkoa wa Singida ni kilomita za mraba 49,341 sawa na asilimia 6 ya eneo la Tanzania Bara ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 11,340 zinafaa kwa kilimo sawa na asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa.
Shughuli za kiuchumi Mkoani Singida ni pamoja na kilimo ambacho huajiri wastani wa asilimia 86 ya wakazi wote.

Mazao ya kipaumbele kwa upande wa chakula ni uwele, mtama, mihogo na viazi vitamu na kwa upande wa mazao ya biashara ni alizeti, vitunguu, pamba na ufuta. Shughuli nyingine za uzalishaji mali ni ufugaji, uchimbaji mdogo wa madini, viwanda vidogo na biashara.

Pato la Mkoa ni Sh. 978,701,000 huku pato la Mwananchi likiwa ni Sh. 697, 667 kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2013.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Singida ni 2,008,058 ikiwa wanaume ni 995,703 na wanawake ni 1,012,355.

Habari Zifananazo

Back to top button