Miaka 61 ya Mapinduzi: Kutoka Karume hadi Dk Mwinyi

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi

LEO ni siku ya kumbukizi ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12, 1964 kwa kuung’oa utawala dhal imu wa kikoloni chini ya Sultani wa mwisho, Jamshid bin Abdullah na kuweka madaraka mikon oni mwa Wazanzibar.

Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotekelezwa chini ya uongozi wa mwasisi wake, Abeid Amani Karume yamelelewa na Watanzania kupitia viongozi mbalimbali wakuu wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbali na Karume, marais wengine walioongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na miaka ya urais wao katika mabano ni Aboud Jumbe (1972 hadi 1984), Ali Hassan Mwinyi (1984 hadi 1985), Idris Abdul Wakil (1985 hadi 1990), Sal min Amour (1990 hadi 2000), Amani Abeid Karume (2000 hadi 2010), Dk Ali Mohamed Shein (2010 hadi 2020) na Dk Hussein Mwinyi (2020 hadi sasa).

Advertisement

Katika kipindi hicho, marais wa Jamhuri ya Muun gano wa Tanzania wame kuwa ni Mwalimu Julius Nyerere (1964 hadi 1985), Ali Hassan Mwinyi (1985 hadi 1995), Benjamin Mkapa (1995 hadi 2005), Jakaya Kikwete (2005 hadi 2015), John Ma gufuli (2015 hadi 2021) na Samia Suluhu Hassan (2021 hadi sasa).

Kimsingi, Mapinduzi ya Zanzibar ni mapinduzi yali yoleta haki, amani, usawa na maendeleo kwa Watanzania yakiwatoa Wazanzibar katika tope la ubaguzi wa wakoloni hususani katika masuala ya haki na huduma za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Mapinduzi yameboresha huduma za kijamii zikiwamo za afya na elimu na hata kujenga usawa na upatanisho visiwani humo yakilenga ku ondoa maadui wa maendeleo yaani umaskini, ujinga, mara dhi na utengano (ubaguzi). Februari 12, 1965 Nyer ere alinukuliwa akisema mapinduzi si hasa suala la kuangusha serikali iliyopo madarakani, bali kubadili hali kwa kuondoa dhuluma na kuweka haki.

“Maisha yageuke, hali iwe nzuri kama watu walikuwa wanyonge, sasa wasiwe wanyonge; kama walikuwa hawasomi (hawapati elimu), yameondoa hali mbaya ya maisha kwa Wazanzibar na kuyafanya kuwa bora zaidi katika nyanja mbalimbali. sasa wasome na kama wa likuwa wanatemewa mate barabarani, sasa wasitemewe…” anasema Nyerere.

Nyerere anakwenda mbali na kusema, “Bila Mapinduzi ya Zanzibar, kusingekuwa na Tanzania hata kidogo…” hii ni kwa kuwa baada ya mapinduzi hayo ya Januari 12, 1964, Zanzibar na Tanganyika ziliungana na kupatikana Tanzania, Aprili 26, 1964.

Karume mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema mapinduzi ni kupindua na kuondoa hali ya unyonge kwa watu na kuwapa tumaini jema na hali bora.

Zanzibar

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba ananukuliwa na kituo kimoja cha televisheni nchini akisema Mapinduzi ya Zanzibar yamelindwa na Wazanzibar tangu yalipoingia katika mikono ya Mwasisi wake, Sheikh Abeid Amani Karume na hadi sasa chini ya Rais wa Awamu ya Nane wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi yapo kwenye mikono salama yakinufaisha Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla.

Kimsingi wakati mapin duzi hayo yakitekelezwa na Wazanzibar chini ya uongozi shupavu wa Karume, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa ikiongozwa na Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanzania).

Hii ni kusema kuwa, Tanganyika (Tanzania Bara) ‘ina mkono mkubwa’ kufani kisha, kutekeleza, kulinda na kulea Mapinduzi ya Zanzibar kupitia marais wote wa awamu sita katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia kwa Nyerere hadi Rais Samia Suluhu Hassan aliyepo madarakani.

Wakongwe wa siasa pamoja na wachambuzi wa masuala ya siasa na historia ya Tanzania wanawapongeza viongozi wote walioongoza Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha wanachochea faida za Mapinduzi ya Zanzibar hadi kuonekana na kujidhihirisha miongoni mwa Watanzania huku wote wakidumisha amani, muungano, mshikamano, utu na umoja wa kitaifa

Kimsingi, Mapinduzi ya Zanzibar yameleta mapinduzi ya elimu Zanzibar na manufaa makubwa kwa umma wa Wazanzibar ndio maana ni muhimu kuyalinda kwa nguvu zote.

Watanzania na hata Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi mwenyewe, Desemba 21, mwaka jana aliweka bayana kuwa, katika kipindi cha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar, nchi imeshuhudia hatua kubwa za maende leo katika miundombinu mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, umeme, maji, barabara, teknolojia, mada raja na bandari.

Alikuwa katika Mahafali ya 10 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) Mbweni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar. Kuelekea Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi karibuni, Rais Samia naye amenukuliwa akiwa katika Shule ya Sekondari Misufini, Bumbwini akisema, “Skuli (shule) hii ni moja ya vielelezo vya kazi kubwa inayo endelea kufanyika kuwaletea wananchi maendeleo katika kila sekta nchini.

Matokeo ya kazi hizi kwenye maisha ya wananchi ndio hasa matunda ya Mapinduzi na Uhuru wetu.” Kama matunda ya Map induzi ya Zanzibar, Serikali chini ya Urais wa Karume, Septemba 23, 1964 alitangaza kutoa elimu bila malipo kwa ubora na kwa usawa bila ubaguzi.

Matunda hayo yameen delea kulindwa na viongozi wote wa nchi waliopata kuwa madarakani. Serikali pia, kupitia awamu mbalimbali za uongozi imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali zenye huduma mbalimbali zikiwamo za kibingwa na kuhakikisha upatikanaji wa dawa na hu duma nyingine za afya kwa kiwango kikubwa na cha ubora wa hali ya juu.

Hadi sasa, Wazanzibar wanatumia ardhi yao kwa shughuli mbalimbali za uza lishajimali kukidhi mahitaji yao ya kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo ni machache miongoni mwa matunda mengi ya kulinda Mapinduzi. Kama sehemu ya matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar, baada ya Aprili 26, 1964 Zanzibar na Tanganyika ziliungana na kuzaa Tanzania moja ambayo watu wake ni wamoja.

Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kila kukicha kama ilivyo kwa Tanzania nzima, ndani ya Zanzibar demokrasia inazidi kustawi ndio maana kila uchaguzi hata vyama vya siasa vya upinzani vinashiriki na kuchaguliwa katika ngazi mbalimbali.

Wazanzibar nao wamekumbatia utamaduni wa kurithishana uongozi kwa amani na kwa kuzingatia katiba iliyopo. Kwa sasa Zanzibar kuna muundo wa uongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iliyomweka madarakani, Maalim Seif Sharrif Hamad (wakati huo akiwa CUF) kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika SMZ mwaka 2010 hadi 2015 chini urais wa Dk Shein kupitia CCM.

Maalim Seif akashika nafasi hiyo tena chini ya urais wa Dk Mwinyi hadi alipofariki dunia Februari 2021, akiwa katika chama cha ACT-Wazalendo.

Kwa sasa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ni Othman Masoud Oth man wa ACT-Wazalendo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ni Hemed Sulei man Abdulla kutoka CCM.

Hii inaonesha ustawi wa demokrasia Zanzibar unazidi kuimarika. Kushirikiana katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ni ishara ya Wazanzi bar kushirikiana kufuta mak ovu na majeraha ya utawala wa kisultani uliomkandam iza Mzanzibar.

Awamu ya Nane inayoongozwa na Dk Hus sein Mwinyi ambayo ndiyo iliyopo madarakani kupitia CCM iliingia madarakani mwaka 2020. Nayo imejikita kuleta mapinduzi ya uchumi hasa uchumi wa buluu ambao si siri, unazidi kunufaisha Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla. Kimsingi, Serikali ya Dk Mwinyi na watangulizi wake inastahili pongezi kwani sasa inazidi kuboresha na kusimamia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, barabara na kuboresha mae neo mbalimbali yakiwamo ya utalii, hali inayozidi kuvutia wawekezaji visiwani humo hasa katika sekta ya utalii na kuboresha huduma za jamii.

Izingatiwe kuwa, Muun gano wa Tanzania umeimari sha amani hususani kwa Wa zanzibar na sasa wanatembea kifua mbele wakijiheshimu, wakiheshimu wageni na kuheshimiana huku wakiwa huru na salama.