Miamba Ulaya yawania saini ya Florian Wirtz

Kiungo wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz.

TETESI za usajaili barani Ulaya zinasema Arsenal, Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid zinashindania kumsajili kiungo mjerumani Florian Wirtz wa Bayer Leverkusen msimu ujao wa majira ya kiangazi huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka pauni mil 125 ili kumuuza mchezaji huyo mwenye umri miaka 21.(Bild – in German)

Barcelona ina matumaini kufikia makubaliano na fowadi wa Brazil Neymar, 32, Januari wakati atakapokuwa huru kuzungumza na klabu mbalimbali kabla mkataba wake na Al-Hilal kumalizika Juni 2025.(Sport – in Spanish)

SOMA: Kishindo cha siku ya mwisho dirisha la usajili Ulaya

Advertisement

Kiungo mhispania wa Real Sociedad, Martin Zubimendi, 25, amesema hajutii kukataa kuhamia Liverpool wakati wa dirisha la uhamisho majira kiangazi.(Mirror)

Arsenal inatarajia kukabiliwa na upinzani toka AC Milan, Inter Milan na Juventus kumsajili fowadi wa Canada na klabu ya Lille, Jonathan David,24. (Football Insider)

Winga wa Borussia Dortmund, Karim Adeyemi,22, anawindwa na Liverpool.

Timu hiyo ya The Merseyside inataka fowadi huyo wa Ujerumani kuchukua nafasi ya Mohamed Salah majira yajayo ya kiangazi. (Sun)

Everton inaweza kufufua nia yake ya kumsajili fowadi wa Paraguay, Miguel Almiron, 30, ambaye huenda akaondoka Newcastle United Januari, 2025. (Teamtalk)