Miji 28 Singida kunufaika huduma ya maji

UTEKELEZAJI wa mradi wa kimkakati wa maji wa miji 28 kwa Manispaa ya Singida unakwenda kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa wateja kwa zaidi asilimia 90 ifikapo mwakani.

Manispaa ya Singida ni miongoni mwa miji inayonufaika na mradi wa kimkakati wa miji 28 unaotekelezwa kwa thamani ya dola za Marekani milioni 500 sawa na zaidi ya Sh trilioni 1 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA), Sebastian Warioba alipokuwa akizungumza na Habari leo kuhusiana na mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa majisafi na huduma ya majitaka.

Alisema SUWASA inatekeleza miradi kadhaa ya kuboreshaji huduma za maji ikiwamo mradi mkubwa wa Miji 28, ambapo umeanza Aprili mwaka huu na utatekelezwa kwa thamani ya Sh bilioni 45.

“Tunaishukuru Serikali kwa utuwezesha kupata mradi huu, mkandarasi ameshaanza kazi tangu Aprili mwaka huu kwa kuanza na kazi ya uchimbaji visima na unatarajia kukamilika ifikapo mwaka 2024 hatua ambayo itafanya huduma ya maji kuwafikia wananchi kwa zaidi ya asilimia 90.”

Kuhusu maeneo ya pembezoni, Warioba alisema mamlaka imewasilisha Wizara ya Maji andiko mradi wenye thamani ya Sh bilioni 3.4.

“Pia kuna miradi inayotekelezwa kutokana na fedha kutoka serikali kuu, tuna kata 18 tumeshafikia kata 16 na kata 2 bado hazijafikiwa, kupitia fedha hizo tunataka kuzifikia kata zilizobaki na zile chache ambazo hazifikiwa kikamilifu nazo zifikiwe.”

Kwa sasa Manispaa ya Singida ina maunganisho ya majisafi 18,000 ambao wanafikiwa na huduma kwa asilimia 78 wakati maeneo ya pembezoni ya miji saba wanafikiwa kwa asilimia 68. Mji hiyo ni Buguno, Njia Panda, Ikungi, Sepuka, Irisia, Puma na Makiungu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

NBC

MAPINDUZI HALISI.PNG
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

NBC TANZA

MAPINDUZI HALISI YA WAPAMBANAJI.PNG
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

NBC RAIS WA TANZANIA NI NYERERE

MAPINDUZI HALISI YA WAPAMBANAJI.PNG
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

NBC RAIS WA TANZANIA NI NYERERE

MAPINDUZI.jpg
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x