‘Mikakati sita kuinua wachimbaji wadogo’

DODOMA: SERIKALI imebainisha mikakati sita ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini.
Akitangaza mikakati hiyo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde leo Mei 9, 2024 amesema, kwanza serikali imepanga kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/serikali-kupiga-jeki-wachimbaji-wadogo/
Pia, mkakati mwingine ni kutoaji leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo, kutoa elimu ya matumIzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija, kutoa huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini Tanzania (STAMICO).
Aidha, mkamkati mwingine ni kuwasaidia wachimbaji wadogo wapate mikopo nafuu kupitia benki mbalimbali na taasisi za fedha.
Mavunde amesema mkakati mwingine ni kutoa fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO kupitia makampuni yaliyoingia makubaliano(MoU) na STAMICO
Mavunde ametangaza mikakati hiyo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Christine Ishengoma aliyetaka kujua mpango wa serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga.