Mikakati utalii wa Kusini wananchi kunufaika

SERIKALI kupitia Bodi ya Utalii(TTB) imeweka mikakati ya kukuza utalii wa Kusini kupitia mradi wa Regrow kwa kutumia watu maarufu na kushiriki katika matamasha na maonesho ambapo mradi huo utaboresha miundombinu na kuwawezesha kiuchumi wananchi wanaozunguka maeneo yaa vivutio kiuchumi.

Akizungumza na HabariLEO ofisa utalii mwandamizi wa TTB, Sane Tobico amesema wanatengeneza mkakati wa masoko wa jumla kwa ajili ya vituo vya Kusini na mkakati wa masoko ya kiutamaduni ambao ni mwongozo kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa mradi.

“Tunatumia watu maarufu kama bongo zozo wanaenda kusini na kuona vivutio na wanaweka kwenye mirandao yao na pia tunashiriki kwenye matamasha na maonesho mbalimbali tunaeleza vivutio vilivyopo kusini.

Amesema pia wanawawezesha wadau wa utalii kwa kuwapa elimu kupitia njia mbalimbali.

“Lengo ni kuwawezesha kukutana na wenzao waliofanikiwa kujifunza namna wanafanya na kupata elimu kupitia semina zinazoendelea katika maonesho hivyo mradi unawawezesha na pia unafanya uwezeshaji wa wataalamu kupata elimu ya Kusini,”amesisitiza.

Amesema kupitia mradi huo sasa watu wameboresha mazao ya utalii hasa watu wa utamaduni wameboresha vifungashio na kuwavutia watalii wengi zaidi

“Wengi wamekuwa wakitembelea vivutio kwa ajili ya kusikia matangazo.

Aidha ameainisha vivutio vya kusini ni vivutio vya asili na hifadhi za Taifa ziko sita ambazo ni Hifadhi za Taifa za Mikumi,Odizungwa ,Nyerere, Ruaha Tulo, Katavi na pia kuna pori za akiba ambazo zina wanyama na maporomoko ya maji.

“Na vivutio vya malikale ni zama za mawe za kale za Isimila, Makubusho ya Kalenga ya chifu Mkwawa,Makubusho ya Iringa Boma ,makubusho ya Songea kwa ajili ya vita vya majimaji na utamaduni wa Kusini.

Kwa upande wake ofisa mwandamizi, Amina Rashid alisema wanajitangaza kupitia kusini mwa Tanzania na huo ni mradi wa Benki ya Dunia ambao lengo lake ni kuendeleza mradi kukuza na kuendeleza wa utalii wa kusini.

Amesema lengo ni kutangaza utalii,kuboresha miundombinu na kuwawezesha kiuchumi wananchi wanaozunguka maeneo yaa vivutio kiuchumi.

“Mradi umejikita kuboresha miundombinu ya utalii ambayo inajumuisha kujenga malazi ndani ya hifadhi na kuboresha barabara, kujenga na kuboresha viwanja vipya vya ndege na kuwezesha ndege kubwa kutua.

Amesema mradi huo unatoa fursa kwa wadau na wawekezaji kukuza kusini kwani ni rahisi kwao kuna vivutio vingi vya kitamaduni na historia, maliasili na maeneo ni makubwa.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button