Benki zakumbwa na mikopo isiyolipika

MOJA ya viashiria vya kudorora kwa uchumi ni uwezo wa wakopaji kurejesha mikopo yao kulingana na masharti ya mikataba yao na taasisi za kifedha. Changamoto za sasa za kiuchumi zinazoikumba Kenya zinaendelea kufichua udhaifu mkubwa wa kiuchumi uliopo nchini humo, hasa katika kipindi cha maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa Kenya ulikuwa ukionekana kuwa imara na wenye ukuaji mzuri. Hata hivyo, sekta ya benki imekuwa ikikumbwa na ongezeko la mikopo chechefu (Non-Performing Loans – NPLs), hali ambayo kiuchumi inaashiria msukosuko katika sekta muhimu za uzalishaji.
Mikopo chechefu ni mikopo ambayo wakopaji wameshindwa kulipa kwa muda wa siku 90 au zaidi. Ongezeko la uwiano wa mikopo chechefu linaonyesha kupungua kwa uwezo wa kurejesha mikopo, upungufu wa ukwasi kwa biashara na hali ngumu ya kiuchumi kwa ujumla.
Ingawa mfumo wa kifedha wa Kenya una mtaji wa kutosha ukilinganishwa na baadhi ya nchi nyingine, kuendelea kuongezeka kwa mikopo chechefu katika sekta mbalimbali kunaashiria changamoto za kimuundo katika uchumi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Kenya, ripoti za kifedha za benki zinaonyesha kuwa uwiano wa mikopo chechefu umeendelea kuwa wa tarakimu mbili kwa miaka kadhaa, wakati mwingine ukizidi asilimia 14. Hali hii imepunguza utoaji wa mikopo mipya na kuongeza shinikizo katika mizania ya benki. SOMA: Uzembe Bandari Mombasa Wapunguza Mapato Kenya
Sekta ya mali isiyohamishika (real estate) imeathirika zaidi. Benki zilifadhili kwa kiasi kikubwa miradi ya makazi na majengo ya biashara wakati wa boom ya ujenzi miaka ya 2010. Hata hivyo, kupungua kwa mahitaji ya nyumba za gharama kubwa, ongezeko la riba na kupungua kwa uwezo wa wananchi kununua kumesababisha mauzo kuchelewa na wakopaji kushindwa kulipa kwa wakati.
Sekta ya viwanda nayo imeathirika kutokana na gharama kubwa za nishati, kupanda kwa bei za malighafi zinazoagizwa kutoka nje na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya. Hali hii imeongeza gharama za uzalishaji na kupunguza faida za kampuni, hivyo kuathiri uwezo wao wa kulipa mikopo. Katika sekta ya biashara ya jumla na rejareja kupungua kwa kipato cha wananchi kutokana na mfumuko wa bei na ongezeko la kodi kumesababisha mauzo kushuka.

Biashara nyingi zinazoendeshwa kwa faida ndogo zimejikuta zikishindwa kurejesha mikopo ya mtaji wa kuendeshea shughuli zao. Kilimo nacho kinaendelea kukumbwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kama ukame na mafuriko, pamoja na kushuka kwa bei za mazao katika soko la dunia. Aidha ucheleweshaji au kusuasua kwa miradi ya umwagiliaji kutokana na changamoto za kiutawala na rushwa kumeathiri uzalishaji na kipato cha wakulima.
Sekta ya ujenzi imeathiriwa na kuchelewa kwa malipo ya miradi ya serikali, jambo linalowaweka wakandarasi katika hali ya upungufu wa fedha na kushindwa kulipa mikopo yao kwa wakati. Sekta ya usafirishaji nayo imekumbwa na kupanda kwa bei ya mafuta na kushuka kwa mizigo bandarini, hali inayoongeza gharama na kupunguza mapato. Sekta ya nishati na huduma za umma inahitaji uwekezaji mkubwa wa awali na muda mrefu wa kurejesha fedha. Hata hivyo, ucheleweshaji wa malipo kwa wazalishaji binafsi wa umeme umeongeza hatari za kifedha.
Biashara ndogo na za kati (SMEs) zimeathirika zaidi kwani mara nyingi hukosa dhamana za kutosha na hutegemea soko la ndani ambalo limepungua. Aidha kaya zinazokopa kwa ajili ya nyumba, magari au matumizi ya kawaida zimekumbwa na shinikizo la gharama za maisha na ongezeko la kodi. Matokeo ya ongezeko la mikopo chechefu ni kupungua kwa ukuaji wa mikopo mipya kwani benki zinakuwa makini zaidi na kuongeza riba ili kujikinga na hatari. Hali hii inapunguza uwekezaji na kasi ya ukuaji wa uchumi.
Kwa ujumla, ongezeko la mikopo chechefu nchini Kenya si takwimu za benki tu bali ni kiashiria cha changamoto za kina za kimuundo katika uchumi. Kukabiliana na hali hii kunahitaji sera madhubuti za uthabiti wa uchumi, usimamizi bora wa fedha za umma, udhibiti wa mfumuko wa bei, usimamizi wa thamani ya sarafu, kuimarisha kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi na mifumo bora ya marekebisho ya mikopo ili kurejesha ukuaji endelevu wa uchumi.




https://youtu.be/KzqoSeVMGrQ?si=glyzAfrc9xTfCn5K
I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com