WAZIRI wa Habari, Mawasiliano Teknolojia Habari, Jerry Silaa amesema jumla ya minara 279 kati ya minara 758 imekamilika na kuwashwa ikiwa ni sawa na asilimia 36 ya utekelezaji wa mradi wote.
Aidha ametoa wito kwa watoa huduma za mawasilinao walioingia mkataba wa ujenzi wa minara kukamilisha kutekelezaji wa mradi huo kabla ya tarehe ya mwisho Mei 13, 2025 ambayo ndio mwisho wa mkataba.
Aidha Waziri Silaa ametoa tahadhari kuwa hakutakuwa na nyonngeza ya muda pindi muda wa mkataba utakapokwisha.
SOMA: Silaa ateua mtendaji mkuu UCSAF
Waziri Silaa amesema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya Tehama kwa walimu 300 wa shule za sekondari katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Hivyo nitumie fursa hii kuwataka wakandarasi wote waliopewa jukumu la kujenga m,inara jhii wananfanyakazi hgii kwa ufanisi mkubwa na kuimaliza kabla ya muda wa mkata kuisha,” Waziri Silaa amesisitiza.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu 100 wa shule za sekondari yaliyofanyika katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) leo tarehe 07 Oktoba 2024 jijini Dar es Salaam.#SmartTanzania #KaziIendelee pic.twitter.com/QiAkyyF30t
— Wizara ya Habari,Mawasiliano naTeknolojia yaHabari (@wizarahmth) October 7, 2024
Waziri Silaa amesema mradi huo unaotekelezwa na serikali unalenga kufikisha huduma za mawasiliano vijijini pamoja na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara huku ukitarajiwa kujenga minara katika kata 713 na vijiji 1,407 huku ukilenga kunufaisha waanchi zaidi ya milion 8.5.