Miradi ya elimu ya Sh bilioni 1.2 yakaguliwa

GEITA: MIRADI ya Sh bilioni 1.2 katika sekta ya elimu wilayani Mbogwe imekaguliwa.

Miradi hiyo imekaguliwa leo Novemba 22, 2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati katika ziara yake ya kukagua utekekezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo.

Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa miradi ya elimu katika shule ya msingi Bunyihuna yenye thamani ya Sh milioni 73, Shule maalum ya mchepuo wa Kiingereza Nyakasaluma inayojengwa kwa Sh milioni 600, shule ya sekondari Bugegere inayojengwa kwa thamani ya Sh milioni 584.

Katika ukaguzi huo Gombati amemuelekeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbogwe kuhakikisha miradi yote inasimamiwa na kukamilika haraka na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia ameagiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili Januari ianze kufanya kazi.

Aidha, amesisitiza usimamizi wa karibu kwenye miradi ndani ya wilaya hiyo na kwamba kumalizika kwa fedha wakati mradi haujaisha ni ishara ya uzembe wa kutosimamia miradi kwa ukaribu. 

Gombati, ameupongeza uongozi wa Mbogwe chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo Sakina Jumanne kwa kuchukua hatua za kisheria na za kinidhamu kwa watendaji ambao hawatimizi wajibu wao ipasavyo na kupelekea serikali kupata hasara kwenye miradi.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button