Mishahara ilipwe kabla ya Eid El Fitr

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameagiza malipo ya mishahara ya mwezi huu kufanyika kuanzia 14 Aprili, 2023 kwa wafanyakazi wa serikali kwa ajili ya matayarisho ya Sikukuu ya Eid El Fitr.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu leo Aprili 16, 2023 inasema kuwa Rais Mwinyi ameagiza malipo hayo yaanze kufanyika kuanzia tarehe hiyo ili kuwapa muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya sikukuu hiyo.

“Pia Rais Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa serikali kwa ushirikiano wao wakati wote wa ibada tangu kuandama kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan”.

Advertisement

Sherehe za Eid El Fitr zinatarajiwa kuangukia kati ya siku ya ijumaa au jumamosi ya tarehe 21 au 22 Aprili 2023 kutokana na kuandama kwa mwezi na kuashiria kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *